Where everything, and anything around YOU and me can be talked about...calling on all my fellow Africans...And if you don't like it, then put something you do like ...
Tuesday, March 6, 2012
Wednesday, October 5, 2011
Friday, September 16, 2011
Wednesday, June 1, 2011
THE NYAMA CHOMA FESTIVAL 2011 PRESS CONFERENCE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMASHA LA NYAMA CHOMA 2011
Dar es Salaam Mei 31, 2011: Tamasha la Nyama Choma litafanyika siku ya jumamosi tarehe 4 juni, kuanzia saa tano na nusu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
Tamasha hili, linakusudia kukuza mahusiano ya kijamii, ukizingatia kwamba nyama choma ni kitoweo kinachopendwa na watanzania wengi, na hivyo hukutanisha watu kutoka makundi yote ndani ya jamii.
Nia kuu, ni kusherehekea kitoweo hiki maarufu, na kuendeleza mahusiano, lakini pia kusaidia wenzetu ndani ya jamii Nusu ya fedha itatolewa kwa njia ya msaada na fedha kwa wenzetu waliokumbwa na maafa ya mabomu ya gongo la mboto.
Tamasha hili linatarajia kufanyika kila mwaka, na limejisajiliwa Brela kama biashara chini ya kanuni na sheria za kampuni na biashara Tanzania. Kila tamasha hili zaidi ya kuwaleta watu pamoja, pia litaangalia jamii yetu ina tatizo gani kwa wakati huo na jinsi gani tunaweza kuwasaidia wenzetu.
Kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa DJ maarufu hapa mjini Dar es Salaam, Bonny Luv, pamoja na michezo ya watoto.
Tamasha hili limedhaminiwa na bia ya Safari Lager, Kinywaji laini cha Coca Cola, na mvinyo wa Dodoma Wine, ambao ndio wamewezesha matayarisho ya tamasha hili.
Baadhi ya sehemu za nyama choma zitazokuwepo ni pamoja na Rose Garden, Fya Tanga, Tanzanian Garden, GBF,Jolly’s Club, Kisumo Bar, Nguruko Bar, Lyimo’s Mbuzi Corner Bar, T-Boners na Kwa Mfojo Bar.
Karibuni wote, tuburudike pamoja, na kusherehekea NYAMA CHOMA kama watanzania halisi.
Saturday, May 14, 2011
SHERIA ZA TAMASHA LA NYAMA CHOMA

SHERIA NA KANUNI ZA TAMASHA LA NYAMA CHOMA 2011.
1. Usafi na kanuni za afya lazima zizingatiwe kwa vyovyote, kutakuwa na afisa afya atayekagua mabanda yote na kuhakikisha vyakula vyote vinatayarishwa kwa hali ya usafi, endapo utakutwa unapuuzia hili, utatolewa kama mshiriki bila kurudishiwa kodi ya banda.
2. Mshiriki anatakiwa kufika kwenye tamasha na vitendea kazi vyote vya matayarisho, vikiwemo vyombo vya kuhifadhia chakula na vya kuuzia wateja.
3. Mshiriki haruhusiwi kuuza vinywaji vya aina yoyote ile.
4. Mshiriki anatakiwa aanze matayarisho ya uaandaaji na upishi masaa sita kabla, geti litafunguliwa saa 5 na nusu asubuhi, hivyo masaa sita kabla.
5. Mshiriki atazingatia usafi wakati wote wa tamasha, na atashiriki katika kuhakikisha banda lake limeachwa safi baada ya shughuli.
6. Mshiriki anatakiwa aahidi kuwa na uwezo wa kilo 60 za Nyama, ambacho ni kima cha chini, unaweza kuja na zaidi ya hiyo. KITIMOTO HAKIRUHUSIWI.
REGISTRATION FORM THE NYAMA CHOMA FESTIVAL
TAMASHA LA NYAMA CHOMA 2011
JUMAMOSI TAREHE 4 JUNI 2011
VIWANJA VYA POSTA, KIJITONYAMA
SAA 11hrs00- 19hrs00
Fomu ya usajili na kukodisha banda la Nyama choma.
JINA MCHOMA NYAMA………………………………………
SIMU NA ANUANI…………………………………………
WILAYA……………………………………………….
IDADI YA BANDA……………………………………………
KIASI CHA NYAMA ZITAKAZOCHOMWA (Kgs)…………..
(kiasi cha chini ni 60kgs)
AINA ZA NYAMA ZITAZOCHOMWA……………………….
MIMI………………………………..KWA NIABA YA……………….. KAMA MSHIRIKI WA TAMASHA LA NYAMA CHOMA NAKUBALI SHERIA NA KANUNI ZA TAMASHA LA NYAMA CHOMA, NAAHIDI KUUZA CHAKULA TU, NA SI VINYWAJI.
JINA……………………………..SAHIHI………………………
JUMAMOSI TAREHE 4 JUNI 2011
VIWANJA VYA POSTA, KIJITONYAMA
SAA 11hrs00- 19hrs00
Fomu ya usajili na kukodisha banda la Nyama choma.
JINA MCHOMA NYAMA………………………………………
SIMU NA ANUANI…………………………………………
WILAYA……………………………………………….
IDADI YA BANDA……………………………………………
KIASI CHA NYAMA ZITAKAZOCHOMWA (Kgs)…………..
(kiasi cha chini ni 60kgs)
AINA ZA NYAMA ZITAZOCHOMWA……………………….
MIMI………………………………..KWA NIABA YA……………….. KAMA MSHIRIKI WA TAMASHA LA NYAMA CHOMA NAKUBALI SHERIA NA KANUNI ZA TAMASHA LA NYAMA CHOMA, NAAHIDI KUUZA CHAKULA TU, NA SI VINYWAJI.
JINA……………………………..SAHIHI………………………
Saturday, April 30, 2011
The Nyama Choma Festival 2011

The Nyama Choma Festival, is a registered event, and will be held once every year, beginning 2011. This one-of-a-kind BBQ extravaganza showcases the best BBQ pitmasters from around the city of Dar es Salaam , a beer garden, and live entertainment.
15 Nyama Choma Pitmasters/ Bars/ Cookouts in Dar, come together on the 4th June 2011 at Kijitonyama Postal Grounds to offer you the best of Nyama Choma...come enjoy BBQ meat, however you want it, while you sip on a cold beer, and get entertained by a live band and artist perfomances!!! Jugglers, Mimics and jumping castles will entertain the kids as grown ups get down to some serious meat eating!!! Come one, Come all!
Opportunities are still open for sponsors, if you are in the food or beverage industry, OR you want to seize this chance to advertise your brand and sell your products to hundreds of Nyama Choma Eaters, do not hesitate to contact us.
call +255 787 28 11 00 or +255 778 44 32 73
or email us ndosicarol@gmail.com
Subscribe to:
Posts (Atom)
