Wednesday, June 1, 2011

THE NYAMA CHOMA FESTIVAL 2011 PRESS CONFERENCE




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMASHA LA NYAMA CHOMA 2011

Dar es Salaam Mei 31, 2011: Tamasha la Nyama Choma litafanyika siku ya jumamosi tarehe 4 juni, kuanzia saa tano na nusu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.

Tamasha hili, linakusudia kukuza mahusiano ya kijamii, ukizingatia kwamba nyama choma ni kitoweo kinachopendwa na watanzania wengi, na hivyo hukutanisha watu kutoka makundi yote ndani ya jamii.

Nia kuu, ni kusherehekea kitoweo hiki maarufu, na kuendeleza mahusiano, lakini pia kusaidia wenzetu ndani ya jamii Nusu ya fedha itatolewa kwa njia ya msaada na fedha kwa wenzetu waliokumbwa na maafa ya mabomu ya gongo la mboto.

Tamasha hili linatarajia kufanyika kila mwaka, na limejisajiliwa Brela kama biashara chini ya kanuni na sheria za kampuni na biashara Tanzania. Kila tamasha hili zaidi ya kuwaleta watu pamoja, pia litaangalia jamii yetu ina tatizo gani kwa wakati huo na jinsi gani tunaweza kuwasaidia wenzetu.

Kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa DJ maarufu hapa mjini Dar es Salaam, Bonny Luv, pamoja na michezo ya watoto.

Tamasha hili limedhaminiwa na bia ya Safari Lager, Kinywaji laini cha Coca Cola, na mvinyo wa Dodoma Wine, ambao ndio wamewezesha matayarisho ya tamasha hili.

Baadhi ya sehemu za nyama choma zitazokuwepo ni pamoja na Rose Garden, Fya Tanga, Tanzanian Garden, GBF,Jolly’s Club, Kisumo Bar, Nguruko Bar, Lyimo’s Mbuzi Corner Bar, T-Boners na Kwa Mfojo Bar.

Karibuni wote, tuburudike pamoja, na kusherehekea NYAMA CHOMA kama watanzania halisi.